• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakosoa visingizio vya India kwa wanajeshi wake kuingia kwenye ardhi ya China

    (GMT+08:00) 2017-08-23 09:36:42

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying, amesema China inatumai kuwa India itachukua hatua za kivitendo kurekebisha vitendo na kauli zake, kufuatia kitendo cha wanajeshi wake kuvuka mpaka na kuingia kwenye ardhi ya China.

    Kauli ya bibi Hua imekuja baada ya kauli ya waziri wa mambo ya ndani wa India Bw Rajnath Singh, ambaye amesema licha ya kuwa India sio nchi korofi na haijawahi kufanya uchokozi, kamwe haitakaa kimya kuhusu usalama wake. Pia amesema suluhu ya mvutano uliopo itapatikana hivi karibuni, na anatarajia kuwa China itachukua hatua chanya.

    Bibi Hua amesisitiza kuwa msingi wa kutatua mvutano wa sasa ni India kuondoa wanajeshi wake na zana zake za kijeshi kutoka upande wa China na kuvirudisha kwenye upande wa India.

    Vyombo vya habari vya India vimeripoti kuwa maofisa wa India na Russia wamejadili suala la mpaka wa India na China, na upande wa India unasema kitendo cha China kujenga barabara karibu na mpaka ni kubadilisha hali ya sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako