• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makataa ya matumizi ya mifuko ya plastiki Kenya yatia wasiwasi wafanyabaishara

    (GMT+08:00) 2017-08-23 18:28:31

    Wafanyabiashara wengi nchini Kenya wana wasiwasi kutokana na ilani ya kupiga marufuku utumizi wa mifuko ya nailoni.

    Halmashauri ya mazingira (NEMA) na serikali imeweka makataa hadi Agosti 28 ya kusitisha utumizi wa mifuko ya nailoni.

    Mwenyekiti wa wafanyabiashara mjini Thika, Bw Alfred Wanyoike, alisema kuwa biashara ndogo ndogo zitaathirika pakubwa kwa vile wengi wao hutumia mifuko hiyo wanapofungia wateja wao bidhaa wanazowauzia.

    Alisema kile kinachostahili kuzingatiwa sana ni utupaji ovyo wa mifuko hiyo kwa vile kufanya hivyo kunachafua mazingira - lakini sio utumiaji wake.

    Alisema jambo muhimu linalostahili kutiliwa maanani zaidi ni kuhamasisha wananchi kuhusu hatua hiyo ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya nailoni.

    Halmashauri ya usimamizi wa mazingira nchini Kenya (NEMA) imetangaza kuwa mapipa ya kutia uchafu na taka hayatakuwa miongoni mwa marufuku ya mifuko ya plastiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako