• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa watoa mafunzo kwa polisi wa Somalia kuhusu uhalifu wa kingono na kijinsia

  (GMT+08:00) 2017-08-23 18:40:26

  Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia imemaliza mafunzo ya siku tatu kwa askari polisi wa nchi hiyo kuhusu uhalifu wa kingono na kijinsia, ili kuwasaidia kukabiliana na tatizo hilo.

  Taarifa iliyotolewa na Tume hiyo imesema, mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa wa maofisa wa usalama kuhusu hatari za uhalifu wa kingono na kijinsia, na vurugu zinazohusiana na uhalifu wa kingono.

  Mafunzo hayo yaliyoandaliwa kwa pamoja na wizara ya wanawake na masuala ya haki za binadamu ya Somalia na Tume hiyo, iliwakutanisha maofisa 54 ambao pia walipata mafunzo kuhusu haki za binadamu na jinsi ya kulinda uhuru wa kundi lililo hatarini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako