• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Neymar kwenda mahakamani kupinga mashtaka yaliowasilishwa na klabu ya Barcelona.

  (GMT+08:00) 2017-08-24 09:03:21

  Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar amesema kuwa ataenda mahakamani kupinga mashtaka yaliowasilishwa na klabu yake ya zamani Barcelona.

  Barcelona inataka Euro milioni 8.5 za marupurupu iliyomlipa mchezaji huyo baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitano miezi tisa kabla ya kuahamia PSG.

  Mchezaji huyo wa Brazil alihamia PSG kwa kitita cha £200m kilichovunja rekodi mnamo mwezi Agosti baada ya kununua mkataba wake.

  Neymar pia anaonekana kusema kuwa Barcelona inafaa kumlipa fedha kufuatia hatua yake ya kuondoka kinyume na inavyodaiwa na timu hiyo.

  Siku ya Jumanne Barcelona ilitaka kulipwa marupurupu iliyomlipa mchezaji huyo baada ya kusaini mkataba mpya pamoja na asilimia 10 ya kucheleweshwa kwa malipo hayo. Klabu hiyo inamtaka mchezaji huyo kurudisha fedha hizo kwa kuwa tayari alikuwa ameshasaini mkataba mpya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako