• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan atoa amri kuharakisha kunyang'anya silaha nyepesi kutoka kwa raia eneo la Darfur

    (GMT+08:00) 2017-08-24 09:31:40

    Rais Omar Al-Bashir wa Sudan amesisitiza kuwa serikali ya Sudan haitavumilia vitendo vinavyoharibu usalama wa taifa katika eneo la Darfur. Kwa sasa jambo muhimu zaidi ni kunyang'anya silaha kutoka kwa raia.

    Bw. Al-Bashir amesema hayo akikutana na gavana wa jimbo la Darfur Kaskazini Bw Abdul-Wahid Yousif, na kusema magavana wa eneo la Darfur wanatakiwa kufanya juhudi kulinda usalama na utulivu wa eneo hilo, kupanga vizuri watu waliopoteza makazi na kushughulikia kwa hatua mwafaka suala la haki za binadamu.

    Habari zinasema tarehe 7 mwezi huu, serikali ya Sudan imetangaza kuanza operesheni ya kunyang'anya silaha na magari yasiyosajiliwa kutoka kwa raia kwenye eneo la Darfur.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako