• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa roboti duniani wa mwaka 2017 wafunguliwa Beijing

    (GMT+08:00) 2017-08-24 09:46:47

    Mkutano wa roboti duniani kwa mwaka 2017 umefunguliwa jana mjini Beijing, China.

    Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, Naibu waziri mkuu wa China Bibi Liu Yandong amesema roboti ikiwa teknolojia ya hali ya juu inayoongoza mustakabali wa dunia, inavumbua sekta mpya na mitindo mipya ya viwanda, na kuleta mageuzi ya kisasa kwa uzalishaji mali na matumizi katika jamii. Amesema serikali ya China inatilia maanani na kuhimiza uvumbuzi katika teknolojia, bidhaa na muundo wa kiviwanda katika sekta hiyo, ili kuziingiza roboti kwa undani kwenye mchakato wa uzalishaji na maisha ya watu.

    Pia ametoa wito kwa nchi mbalimbali kutumia kwa pamoja fursa hiyo ya kihistoria, kuimarisha ushirikiano katika kufanya uvumbuzi katika sekta hiyo, kuhimiza utafiti wa kisayansi, kuwaandaa wataalamu na kupeana uzoefu uliopatikana katika sekta ya uvumbuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako