• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Benki ya Equity kuondoa mikopo ya walioajiriwa

    (GMT+08:00) 2017-08-24 18:45:21

    Wafanyikazi walioajiriwa na kulipwa na payslip sasa huenda wakakosa mikopo baada ya benki ya Equity kutangaza kusitisha huduma hiyo.

    James Mwangi afisa mkuu wa benki hiyo amesema wataondoa mikopo ya mikopo yanayokosa usalama ili kuounguza hasara zinazotokana na wateja wanaofutwa kazi ghafla.

    Mwangi amesema mikopo inayotolewa kwa wateja wake wan chi ya Uganda,Kenya na Tanzania sasa itasitishwa huku akisema pia wafanyibiashara wadogo wadogo aidha hawatapewa mikopo .

    Hatua hii inajiri kufuatia agizo la benki kuu ya Kenya ya riba ya asilimia 7 kiwango ambacho kwa benki za biashara faida yao ya mikopo itapungua.

    Benki ya Equity ina wateja milioni 11.7 Kenya na mwaka huu faida yake imepungua kwa asilimia 7.4 kufuatia kushuka kwa viwango vya riba kwa mikopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako