• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Cristiano Ronaldo atangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya

  (GMT+08:00) 2017-08-25 09:24:00

  Baada ya Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA jana mjini Monaco Ufaransa kuchezesha droo ya hatua ya makundi ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018, walitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya 2016/2017.

  Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno anayeichezea Real Madrid Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya 2016/2017 kwa kumshinda mpinzani wake mkubwa Lionel Messi wa FC Barcelona na golikipa wa Juventus Buffon.

  Ronaldo kwa msimu wa 2016/2017 ambaye pia ameshinda tuzo ya mshambuliaji bora 2016/2017, alikuwa msaada mkubwa kwa club yake ya Real Madrid msimu uliomalizika lakini ameifungia magoli 12 na kusaidia kufunga mara 6 katika michuano ya UEFA Champions League.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako