• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakabiliana na changamoto ya ulemavu

    (GMT+08:00) 2017-08-25 17:37:56

    Leo ni siku ya kwanza ya kukinga ulemavu nchini China. Shirikisho la walemavu la China hivi karibuni limeanza hatua nne za kukinga ulemavu, na kutoa vifungu 30 vya elimu kuhusu namna ya kukinga ulemavu wa kurithi, maradhi na majeraha, na kuboresha huduma kwa watu wenye ulemavu.

    Takwimu zinaonesha kuwa, hivi sasa idadi ya watu wenye ulemavu nchini China imezidi milioni 85. China inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuzuia kutokea kwa ulemavu. Mkurugenzi wa idara ya kuponesha ya shirikisho la walemavu la China Bw. Hu Xiangyang, ameeleza kuwa kila mtu ana uwezekano wa kuwa na ulemevu, hivyo watu wote wanapaswa kutilia maanani kazi ya kuzuia kutokea kwa ulemavu. Kuanzishwa kwa siku ya kukinga ulemavu kutawahimiza watu watambue umuhimu wa kazi hiyo. Anasema,

    "Tunapaswa kuwahimiza watu wote kutilia maanani kazi ya kukinga ulemavu, na kuwafahamisha kuwa kazi hiyo si kama tu inawahusu watu wenye ulemavu, bali pia inawahusu watu wote. Tutatangaza elimu ya kukinga ulemevu, na kuwaelimisha watu kujua hatari kuu za kusababisha ulemavu, na njia mwafaka za kukinga ulemavu."

    Naibu mkurugenzi wa idara ya kuponesha ya shirikisho la walemavu la China Bi Na Xin amesema, kila mwaka idadi ya watoto laki tisa wanazaliwa na ulemavu nchini China. Mbali na hayo ongezeko la maradhi sugu yakiwemo maradhi ya mishipa ya moyo na ubongo, maradhi ya akili linaleta hatari kubwa ya kutokea kwa ulemavu. Ili kuwafahamisha watu njia za kukinga ulemavu, shirikisho hilo limetoa vifungu 30 vya elimu kuhusu namna ya kukinga ulemavu unaotokana na urithi, maradhi na majeraha, na kuboresha huduma kwa watu wenye ulemavu.

    Kwa mfano wa sababu ya urithi, wanawake wanapaswa kuwa makini kabla ya kuwa na uja uzito, na kuepuka kuwa na mimba wakati wa umri mkubwa, wanawake na wanaume wakitaka kuwa na mtoto, wanapaswa kuacha kabisa tumbabu na pombe na vitu vingine venye sumu, na kufanya ukaguzi kiafya. Bi Na Xin anasema,

    "Pia tunatakiwa kufanya juhudi za kukinga ulemavu unaosababishwa na maradhi, haswa maradhi ya kuambukiza, maradhi sugu na maradhi ya akili, na kuhimiza njia bora ya maisha. Aidha tunapaswa kuchukua hatua zaidi za kukinga ulemavu wa watoto na wazee kutokana na majeruhi. Zaidi ya hayo, tutaboresha huduma za kuponesha walemavu, na kuwapatia zana za kufanya mazoezi na mazingira bora ya kijamii."

    Katika siku hiyo ya kukinga ulemavu, China imefanya shughuli mbalimbali zinazohusika, zikiwemo makongamano na semina kuhusu elimu za kukinga ulemavu. Na mashirika ya televisheni ya baadhi ya miji na mikoa ikiwemo Beijing, Shanghai na Liaoning, pia ya na vipindi kuhusu elimu hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako