• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ushirikiano kati ya China na Saudia kuingia zama ya mafanikio zaidi

  (GMT+08:00) 2017-08-25 18:03:59

  Naibu waziri mkuu wa China Zhang Gaoli amesema kuwa anaamini ushirikiano kati ya China na Saudi Arabia utaingia kwenye zama mpya, kuwa mpana zaidi, wa kudumu na wa mafanikio.

  China na Saudia zimefikia makubaliano mapana ya ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali kama vile nishati, fedha, na uwezo wa uzalishaji na pia kwenye miradi muhimu ya ushirikiano.

  Makubaliano hayo yalifikiwa wakati Bw. Zhang alipokutana na Mfalme wa Saudia Salman bin Abdulaziz Al Saud mjini Jeddah. Zhang amesema, ziara yake nchini humo inalenga kutekeleza umuhimu wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya rais Xi Jinping wa China na Mfalme Salman wa Saudia, ili kuendeleza nguvu ya uhusiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Saudia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako