• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa msaada wa makontena matatu ya vyombo vya ukaguzi kwa Kenya

  (GMT+08:00) 2017-08-26 18:34:58

  China imetoa msaada wa makontena matatu ya vyombo vya ukaguzi kwa serikali ya Kenya kwenye bandari ya Mombasa ili kuisaidia Kenya kuongeza uwezo wa kufanya ukaguzi na ufanisi wa kupitisha watu na mizigo kwenye forodha.

  Kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo, kansela wa uchumi na biashara wa ubalozi wa China nchini Kenya Bw. Guo Ce amesema msaada huo ni utekelezaji wa miradi 10 mikubwa ya kutoa misaada kwa Afrika iliyotangazwa na rais Xi Jinping kwenye mkutano wa wakuu wa ushirikiano kati ya China na Afrika mjini Johannesburg Afika Kusini mwaka 2015, pia ni mradi muhimu wa kuisaidia Kenya kutimiza mpango wa muda mrefu wa mwaka 2030.

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya mapato Kenya (KRA) Bw. John Karimi Njiraini amepokea msaada huo na kutoa shukrani kwa China kwa niaba ya serikali ya Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako