• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mwenyekiti wa IOC

    (GMT+08:00) 2017-08-28 09:37:57

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenyekiti wa kamati ya Olimpiki ya kimataifa Bw Thomas Bach na mwenyekiti wa baraza la Olimpiki la Asia Bw Ahmed Al-Sabah ambao wako China kuhudhuria ufunguzi wa michezo ya 13 ya taifa la China.

    Rais Xi Jinping amesema maandalizi ya michezo ya olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing yanaendelea, na China itatekeleza ahadi zote ilizotoa. Amesema China itatumia fursa ya kuandaa michezo hiyo kuhimiza maendeleo yenye uwiano ya michezo ya umma na michezo ya mashindano, na kuinua kiwango cha afya kwa watu wa China.

    Kwa upande wake Bw. Bach amesema ana imani kuwa serikali ya China itafanikisha michezo hiyo kwa teknolojia ya juu na bila uchafuzi na ufujaji.

    Naye Bw. Ahmed amesema, baraza la Olimpiki la Asia litashirikiana na China kuendeleza shughuli za michezo barani Asia, na kuiunga mkono China kuandaa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya mwaka 2022 na michezo ya Asia itakayofanyika Hangzhou.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako