• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Duru ya tatu ya mazungumzo ya Brexit yaanza Brussels

    (GMT+08:00) 2017-08-29 09:44:53

    Uingereza na Umoja wa Ulaya wamezindua duru ya tatu ya mazungumzo ya siku nne kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya mjini Brussels, kujadili masuala ya malipo ya Brexit, maslahi ya raia wa Umoja wa Ulaya na mpaka wa Ireland Kaskazini.

    Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo ya Brexit Bw Michel Barnier amesisitiza kuwa hakuna muda mwingi unaobaki kwa ajili ya kutatua masuala yaliyopo, na kusema Umoja wa Ulaya unafurahia kutolewa kwa waraka wa msimamo wa Uingereza, na kuitaka Uingereza iondoe mapema sehemu zisizo bayana kwenye msimamo wake.

    Mwakilishi wa Uingereza anayeshughulikia mambo ya Brexit Bw David Davis amesema waraka uliotolewa na Uingereza mwezi huu ni matokeo ya juhudi za mwaka mzima uliopita, na unatarajiwa kuweka msingi kwa ajili ya mazungumzo ya kiujenzi ya wiki hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako