• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa nchi za Afrika na Ulaya wakutana Paris kujadili suala la uhamiaji

    (GMT+08:00) 2017-08-29 09:45:17

    Viongozi wa nchi za Afrika na Ulaya wamekutana mjini Paris kujadili suala la uhamiaji, ambapo wamekubaliana kuimarisha uungaji mkono kwa nchi zinazopokea wakimbizi wa Afrika, na kuongeza nguvu za kupambana na uhamiaji haramu.

    Viongozi wa Ufaransa, Ujerumani, Italia, Hispania, Chad, Niger, Libya pamoja na wajumbe wa Umoja wa Ulaya wamehudhuria mkutano huo.

    Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema nchi husika zinatakiwa kuchukua hatua zenye ufanisi kukabiliana na changamoto za pamoja. Nchi za Ulaya zitaimarisha ushirikiano na nchi zinazotoa na zinazopokea wahamiaji, kuwakamata wafanya biashara ya uhamiaji haramu, na kuimarisha usalama na utekelezaji wa sheria.

    Mbali na hayo, viongozi hao pia wameamua kuimarisha uungaji mkono kwa Niger na Chad, na kuhimiza hatua za pamoja za kurejesha utulivu wa kisiasa nchini Libya. Ufaransa, Ujerumani, Italia na Hispania zimeahidi kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kuboresha maisha ya watu wa nchi zinazotoa wakimbizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako