• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Kiwanda nguo cha Burera kufungua zaidi ya nafasi 600 za ajira.

    (GMT+08:00) 2017-08-29 20:31:17

    Kiwanda kipya cha kutengeneza nguo cha Burera nchini Rwanda kinatarajiwa kufungua zaidi ya nafasi 600 za ajira.

    Kiwanda hicho cha Burera ni ubia kati ya wilaya ya Burera na kampuni ya Noguchi Holding ya Japan.

    Kiwanda hicho kinatarajiwa kuanza oparesheni hivi karibuni kikitarajiwa kusuma mbele juhudi za erikali ya Rwanda ya kuwa na bidhaa za kutengenezwa ndani ya nchi.

    Mkurungezi wa kiwanda hicho Jean Marie Niyonzima, amesema serikali inalenga kusaidia watu 200,000 kuwa na ajira ambazo sio za kilimo ifikapo mwaka 2018 na kiwana hicho ni sehemu ya juhudi za kufikia lengo hilo.

    Niyonzima amesema uwekezaji wa kwanza wa franc bilioni 1 huku wilaya hiyo ikiwa na mgao wa mtaji wa asilimia 48 nayo kampuni hiyo ya Noguchi ikichangia asilimia 52.

    Kwa sasa kuna mashine 280 za kisasa kwenye kiwanda hicho za gharama ya franc milioni 170.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako