• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakenya watii marufuku ya mifuko ya plastiki

    (GMT+08:00) 2017-08-30 09:02:33

    Wakenya wameonekana kukumbatia marufuku ya mifuko ya plastiki iliyoanza kutekelezwa jumatatu nchini humo.

    Wafanyabiashara wengi wadogo pamoja na wanunuzi wameanza kutumia mifuko mipya iliyopendekezwa ambayo haiharibu mazingira.

    Katika sehemu nyingi nchini Kenya,wateja walionekana wakibeba mifuko iliyo rafiki kwa mazingira kama vile vyondo vinavyotengenezwa kwa nyuzi za mkonge,na aina nyengine za mifuko tangu marufuku ya mifuko ya plastiki kuanza rasmi jumatatu iliyopita.

    Imekuwa vigumu sana kuona mtu yoyote akiwa amebeba mifuko ya plastiki.

    Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira (NEMA) imetuma maafisa wake katika sehemu mbalimbali jijini Nairobi kufuatilia kuhusu utekelezaji wa marufuku ya mifuko ya plastiki.

    Hawa hapa ni baadhi ya wakenya ambao wameipokea marufuku hiyo kwa mikono miwili wakisema mifuko ya plastiki inaharibu mazingira.

    SAUTI

    Hata hivyo baadhi ya wakenya wanalalama wakisema marufuku hiyo imewakosesha ajira na njia rahisi za kufunga na kubeba bidhaa.

    SAUTI

    Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa Mamlaka ya NEMA Evans Nyabuto amesema Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mazingira,NEMA,Profesa Geoffrey Wahungu ametuma timu ya maafisa kwenda katika viwanda na maduka ili kuangalia iwapo marufuku ya mifuko ya plastiki inatekelezwa,na kuwashauri ambao hawajaanza kutekeleza marufuku hiyo kuanza mara moja.

    Hata hivyo Nyabuto amesema Mamlaka ya Mazingira haikamati watu kwa kutotekeleza marufuku lakini wanawashauri na kuhakikisha kwamba sheria hiyo inafuatwa.

    "Hakuna mpango wowote wa maafisa wa polisi kuanza kuwakamata wananchi.Tafadhalini pigeni ripoti kwa NEMA iwapo kuna maafisa wowote wa polisi wanaokama watu.Tunashirikiana na Inspekta Mkuu wa Polisi kuhusu marufuku hii,na kazi yao ni kuhakikisha usalama wa maafisa wetu wanapokuwa kazini"

    Faini ya shilingi milioni 4 au miaka miwili jela inawasubiri watakaovunja sheria.

    Kulingana na NEMA,faini hiyo kubwa na kifungo ni kwa ajili ya watengenezaji na wauzaji rejareja.

    Baadae serikali ya kaunti itajadili faini atakayotozwa mwananchi wa kawaida atakayepatikana na mifuko ya plastiki.

    Marufuku hii ya mifuko ya plastiki ambayo ilitangazwa na Waziri wa Mazingira Profesa Judi Wakhungu tarehe 28 Februari,ilianza rasmi tarehe 28 Agosti.

    Walindaji mazingira wamempongeza Profesa Wakhungu kwa marufuku hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako