Waziri wa ulinzi wa Iran Bw. Amir Hatami amesema Iran itaendelea kuendeleza teknolojia ya makombora, na hivi sasa uwezo wa makombora ya Iran unaridhisha na uwezo wa kujilinda wa Iran hautabaki nyuma ya madui zake. Mwazoni mwa Agosti, Marekani iliamua kuiwekea vikwazo Iran kutokana na mpango wake wa kuendeleza makombora. Ili kujibu hatua hiyo, bunge la Iran ilipitisha azimio Agosti 13 na kuamua kutenga dola milioni 500 zaidi kwa ajili ya utafiti wa teknolojia ya makombora.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |