• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chansela wa Ujerumani aukosoa Umoja wa Ulaya kwa kutoshughulikia vizuri msukosuko wa wakimbizi

    (GMT+08:00) 2017-08-30 09:41:04

    Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel ameulaumu Umoja wa Ulaya kwa kutoshughulikia vizuri msukosuko wa wakimbizi uliotokea mwaka 2015, na kutoa wito wa kuweka mpango wenye usawa wa kupokea wakimbizi na kuzipatia nchi za Afrika misaada zaidi.

    Katika mkutano na waandishi wa habari, Bibi Merkel amesema Umoja wa Ulaya haukufanya kazi nzuri kwenye suala la wakimbizi, na bado hakuna mpango wenye usawa kwa nchi wanachama wa umoja huo zinazowapokea wakimbizi.

    Bibi Merkel ameongeza kuwa Ujerumani inatakiwa kushirikiana na nchi nyingine katika utatuzi wa suala la wakimbizi. Nchi husika zinatakiwa kuwasiliana na nchi jirani na kuzisaidia kutatua suala la maendeleo ya kiuchumi, ili kudumisha ustawi na utulivu wa Ulaya. Amesema nchi za Ulaya zinatakiwa kufikia makubaliano na nchi za Afrika, na kuzipatia misaada mingi zaidi ya kimaendeleo na kibinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako