• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani na Japan kuongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-08-30 09:48:47

    Viongozi wa Marekani na Japan wametangaza kuongeza shinikizo kwa Korea ya Kaskazini, na kulitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa likutane kujadili suala la Korea Kaskazini kurusha kombora.

    Ikulu ya Marekani imetoa taarifa ikisema, rais Donald Trump wa Marekani na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe wamekubaliana kuwa Korea ya Kaskazini inatishia usalama wa Marekani, Japan na Korea Kusini pamoja na nchi nyingine duniani.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pia ametoa taarifa akieleza kuwa hatua ya Korea Kaskazini imeenda kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa. Ofisa wa umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama Bibi Federica Mogherini ametangaza kuwa Umoja wa Ulaya utafanya majadiliano na wenzi wake kwa mujibu wa matokeo ya majadiliano ya Baraza la Usalama, ili kuamua hatua zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako