• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya aitaka mahakama kuu kufuta ombi la Odinga kuchunguza uchaguzi mkuu

    (GMT+08:00) 2017-08-30 09:55:09

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameitaka mahakama kuu iondoe ombi la kufanya uchunguzi kuhusu uchaguzi mkuu lililotolewa na mpinzani wake Bw. Raila Odinga kutokana na kukosekana kwa ushahidi unaoaminika.

    Wanasheria wa rais Kenyatta wamewaambia majaji huko Nairobi kuwa ombi la Bw Odinga linatokana na uvumi na madai yasiyo na msingi, ambayo kiongozi huyo wa upinzani ameshindwa kuyathibitisha.

    Mwanasheria wa Kenyatta Bw. Ahmednasir Abdulahi amesema, hata kwa kulingana na kiwango cha chini zaidi cha ushahidi unaohitajika, ombi hilo litatupiliwa mbali.

    Katika ombi lake, Bw. Odinga ameitaka tume ya uchaguzi kufuta matokeo ya uchaguzi kutokana na kumpendelea mpinzani wake Kenyatta katika uchaguzi huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako