• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 28 wafariki kutokana na maporomoko ya udongo DRC

    (GMT+08:00) 2017-08-30 10:00:04

    Watu wasiopungua 28 wamefariki dunia kutokana na maporomoko ya udongo yaliyotokea jana huko Kolwezi, mkoani Lualaba, kusini mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

    Gavana wa sehemu hiyo Richard Muyej amesema, maporomoko hayo yalitokea jana mchana kwenye eneo la kampuni moja ya madini. Ameongeza kuwa idadi ya vifo haijathibitishwa kwa kuwa baadhi ya watu wamefukiwa na kifusi cha udongo, na kazi ya uokoaji bado inaendelea.

    Tukio hilo limetokea wiki mbili baada ya watu 200 kupoteza maisha yao katika jimbo la Ituri, na Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo alitangaza siku mbili za maombolezo kuanzia jumatatu kutokana na ajali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako