• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yaahidi kutoa uungaji mkono zaidi kwa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2017-08-30 10:03:32

    Serikali ya Rwanda imeahidi kuendelea kuunga mkono operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa kote duniani.

    Waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Bw. James Kabarebe alisema hayo wakati akitoa hotuba katika mkutano wa maandalizi ya operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa uliofanyika huko Kigali.

    Wajumbe zaidi ya 100 kutoka vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na nchi zinazochangia fedha, wamehudhuria mkutano huo wa siku mbili uliofunguliwa jana, ili kujadili njia za kuboresha ulinzi wa amani.

    Wajumbe hao wamejadili kuhusu kuwalinda watu walio hatarini, kutoa tahadhari ya mapema na kutuma askari haraka.

    Bw. Kabarebe amesema Rwanda imefanya juhudi kubwa katika kuimarisha operesheni za kulinda amani ndani na nje ya Afrika, na nchi hiyo inaahidi kutoa uungaji mkono zaidi kwenye operesheni hizo kote duniani.

    Kwa mujibu wa waziri huyo, Rwanda imetoa uungaji mkono kwa operesheni hizo ikiwemo vikosi, polisi na vifaa kuimarisha nguvu ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako