• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CASS yasema ujenzi wa maeneo ya viwanda ni mbinu muhimu ya ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2017-08-30 10:34:19

    Idara ya utafiti wa Asia magharibi na Afrika katika Taasisi ya sayansi za kijamii ya China CASS imetoa ripoti kuhusu maendeleo ya Afrika ya mwaka 2016-2017, inayotaja ujenzi wa maeneo ya viwanda kuwa ni mbinu muhimu ya ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Afrika.

    Ripoti inasema baada ya kuingia kwa karne ya 21, nchi za Afrika zinajitahidi kusukuma mbele mchakato wa maendeleo ya viwanda, na ujenzi wa maeneo ya viwanda unachukuliwa na nchi nyingi za Afrika kama hatua muhimu ya kuhimiza mchakato huo. Ushirikiano wa uzalishaji viwandani kati ya China na Afrika umepata fursa nzuri ya kihistoria kwa kupitia ujenzi wa maeneo ya viwanda.

    Mpaka sasa, karibu maeneo 100 ya viwanda yamejengwa, yanajengwa au yanapangwa kujengwa barani Afrika, maeneo 30 kati ya hayo yameanza kufanya kazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako