• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa Iraq asema uamuzi wa kupiga kura za maoni katika jimbo la wakurd umekiuka katiba

  (GMT+08:00) 2017-08-30 11:01:11

  Waziri mkuu wa Iraq Bw Haider al-Abadi amesema uamuzi wa serikali ya jimbo la Kirkuk wa kupiga kura za maoni kuhusu kujitenga na Iraq, umekiuka katiba.

  Akikutana na wanahabari, Bw Al-Abadi amesema upigaji kura huo unakiuka katiba, na haupaswi kuidhinishwa na upande mmoja. Ametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ili kutatua masuala yaliyobaki kati ya serikali kuu ya Iraq na jimbo linalojitawala la Kirkuk.

  Kiongozi wa chama cha wakurd katika bunge la Jimbo la Kirkuk Bw Ahmed al-Askari amesema kwamba wabunge 24 kati ya wote 26 walipiga kura ya ndiyo na wengine wawili hawakupiga kura, na hivyo kupitisha uamuzi wa kupiga kura za maoni Septemba 25.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako