• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UNICEF na Rwanda zaunganisha nguvu ya kupambana na ajira kwa watoto kwenye sekta ya chai

  (GMT+08:00) 2017-08-30 16:50:05

  Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesaini makubaliano na Bodi ya Maendeleo ya Usafirishaji wa Mazao ya Kilimo ya Rwanda yanayolenga kusimamisha ajira kwa watoto katika sekta ya chai.

  Mwakilishi wa UNICEF nchini Rwanda Ted Maly amesema, chini ya makubaliano hayo yaliyosainiwa jana, UNICEF itatoa mafunzo ya kitaalam kwa wafanyakazi wa sekta ya chai nchini Rwanda, hivyo kuisaidia nchi hiyo kuboresha ustawi wa watoto na wakina mama.

  Makubaliano hayo yanaendana na ahadi ya serikali ya Rwanda ya kulinda haki ya watoto ya kulindwa, kuhudumiwa, na usalama, bila kujali hali ya kiuchumi ya wazazi wao.

  Kati ya mwaka 2014 na 2016, watoto 2,700 walitolewa kwenye sekta ya chai walikokuwa wakifanya kazi na kurejeshwa shuleni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako