• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitisha mkutano na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa nchi za BRICS
     

    (GMT+08:00) 2017-08-30 16:52:15

    Wizara ya mambo ya nje ya China leo imeitisha mkutano na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa nchi za BRICS utakaofanyika mjini Xiamen China.

    Waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi ameeleza ajenda ya mkutano huo, na kusema kuanzishwa kwa mfumo wa nchi za BRICS ni matokeo ya mabadiliko ya hali na nguvu za nchi duniani, na unaonesha ongezeko la hadhi na ushawishi wa nchi zinazoendelea katika utawala wa dunia. Amesema kutokana na jitihada za pamoja, mkutano wa Xiamen utafungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya nchi za BRICS, na kuacha kumbukumbu katika historia.

    Amesema, mwaka huu ni mwanzo wa mwongo wa pili wa ushirikiano kati ya nchi za BRICS, na kutokana na mabadiliko ya kutatanisha ya hali ya dunia, kundi hilo lina majukumu na uwezo wa kufanya kazi ya kiujenzi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto mbalimbali. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi wanachama wa BRICS kuimarisha zaidi ushirikiano kati yao, ili kunufaisha nchi hizo tano na dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako