• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafafanua msimamo wake katika suala la ulinzi wa amani

    (GMT+08:00) 2017-08-30 18:28:13

    Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi ameeleza msimamo wa China kuhusu operesheni za ulinzi wa amani.

    Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu opresheni ya kulinda amani, Balozi Liu amesema, ingawa kazi za Umoja huo za kuzuia vita, kulinda amani, kujenga amani na kudumisha amani endelevu zina umaalum wake, lakini zinapaswa kufanyika chini ya mtazamo wa pamoja. Amesema, katika miaka ya hivi karibuni, Umoja wa Afrika umepata matokeo mazuri katika kusukuma mbele ushirikiano wa nchi za Afrika kupata amani na maendeleo. China inatarajia Umoja wa Mataifa utaimarisha ushirikiano na Umoja wa Afrika katika kuzuia vita, kudhibiti migogoro, na kazi za ukarabati. Pia amesema, China inapenda kushirikiana zaidi na nchi za Afrika chini ya pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja na kuisaidia kupata amani, utulivu na maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako