• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani Korea Kaskazini kurusha makombora

    (GMT+08:00) 2017-08-30 18:28:31

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeilaani vikali Korea Kaskazini kwa kufanya majaribio ya makombora na kuitaka nchi hiyo kufuata kwa makini maazimio husika ya Umoja huo na kusimamisha majaribio hayo.

    Taarifa ya mwenyekiti wa Umoja huo imesema, kitendo hicho cha Korea Kaskazini kinatishia usalama wa kikanda, pia ni tishio kwa nchi wanachama wa Umoja huo. Pia imetaka Korea Kaskazini kuacha mpango wowote wa nyuklia na silaha za maangamizi, na kusisitiza kuwa Baraza hilo limeahidi kutatua suala hilo kwa njia ya kisiasa.

    Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi amesema, China inapinga kitendo hicho cha Korea Kaskazini kinachokiuka azimio la baraza hilo. China imetoa wito kwa pande zote husika kujizuia, kuacha kitendo chochote cha kuchochea na kulinda amani na utulivu wa peninsula ya Korea kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako