• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Wafanyabiashara wasema marufuku ya mifuko ya plastiki yawapatia hasara

    (GMT+08:00) 2017-08-30 20:02:01

    Wafanyabiashara nchini Kenya wanalalamika kuwa marufuku ya mifuko ya plastiki iliyoanza jumatatu imeathiri biashara zao.

    Baadhi ya wafanyabiashara wanasema mifuko mbadala iliyopendekezwa ni ghali mno na imewaongezea gharama za ziada.

    Wafanyabiashara hao wanasema awali walinunua mifuko 100 ya plastikikwa Sh50 ilhali sasa wanalazimika kununua 64 ya kaki kwa Sh250 ili kutii marufuku ya mifuko ya plastiki.

    Wanalalama kuwa gharama hiyo ni ghali mno.

    Wakati huo huo, Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (NEMA) jana ilifafanua kuwa maafisa wake bado hawajaanza kuwatia nguvuni wanaokiuka marufuku dhidi ya mifuko ya plastiki.

    NEMA ilieleza kuwa kile wanachofanya kwa sasa ni kuwaonya wakosaji, lakini wataanza kuwakamata watu hivi karibuni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako