• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni ya mawe yaunganisha masoko ya nchi za BRICS

    (GMT+08:00) 2017-08-30 20:22:03

    Katika mji wa pwani wa Xiamen ulioko kusini mashariki mwa China kuna kampuni inayoshughulikia uchimbaji wa mawe, utengenezaji wa bidhaa za mawe na biashara ya mawe. Kampuni hii iitwayo WanliStone si kama tu imeanzisha shughuli zake mjini Xiamen na miji mbalimbali nchini China, bali pia imeanzisha biashara na nchi na sehemu 30 zikiwemo nchi za Afrika.

    Kampuni ya WanliStone iliyoanzishwa mwaka 1996 ilitupia macho soko la Afrika mapema. Si kama tu inafanya biashara ya mawe nchini Afrika Kusini, bali pia imeanzisha ushirikiano wa kiwenzi na makampuni ya nchi hiyo. Mwaka 2003, ili kupanua shughuli zake barani Afrika, kampuni hiyo ilianzisha kiwanda cha utengenezaji wa bidhaa za mawe nchini Afrika Kusini, na hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa makampuni ya mawe ya China kuanzisha kiwanda cha aina hiyo katika nchi za nje. Alipozungumzia sababu ya kuchagua Afrika Kusini kuanzisha kiwanda chake, meneja mkuu Bw. Hu Jingpei anasema,

    "Afrika Kusini ina rasilimali nyingi za mawe, hasa mawe meusi, ambayo ni maarufu duniani. Tena Afrika Kusini ni nchi muhimu kusini mwa bara la Afrika, tunaweza kuingia kwenye soko zima la kusini mwa Afrika kupitia Afrika Kusini ambayo ina umuhimu wa kijiografia."

    Mwanzoni kampuni ya WanliStone ilifanya majaribio ya kuwekeza nchini Afrika Kusini, lakini baadaye iligundua mustakabali mzuri wa soko la Afrika. Hivi sasa si kama tu imeanzisha shughuli zake kusini mwa Afrika, bali pia imeingia kwenye masoko ya Ethiopia, Kenya, Zimbabwe n.k, katika siku zijazo huenda itajenga kiwanda kipya Afrika Mashariki. Bw. Hu anasema,

    "Licha ya Afrika Kusini, tumejenga kituo cha utengenezaji nchini Algeria kwa kushirikiana na kampuni ya ujenzi na uhandisi ya China CSCEC. Na tumeanzisha mradi nchini Kenya. Mawe yetu pia yametumiwa kwenye ujenzi ya jengo la makao makuu ya Umoja wa Afrika nchini Ethiopia. Ingawa hatujajenga viwanda katika eneo la Afrika ya Kati na Afrika Mashariki, lakini tumeanzisha biashara huko, tutashiriki kwenye mradi wa uwanja wa ndege nchini Angola na miradi kadhaa ya kibiashara nchini Kenya."

    Wakati kampuni yake ilipoingia kwenye soko la Afrika Kusini, Bw. Hu aligundua kuwa kutokana na ukosefu wa teknolojia, nchi hiyo haiwezi kutumia rasilimali ya mawe kwa ufanisi mkubwa. Hivyo kampuni yake inashikilia kuwaajiri wafanyakazi wa Afrika Kusini, na kuwapatia mafunzo, ili kuendana vizuri na soko la huko, na kutoa nafasi nyingi zaidi za ajira kwa nchi hiyo na nchi jirani. Bw. Hu anasema,

    "Mwanzoni tuliajiri wafanyakazi 50 wa Afrika Kusini, na kuwaleta hapa China ili wapate mafunzo kwa nusu mwaka. Miongoni mwa makampuni mengi ya China nchini Afrika Kusini, kampuni yetu ina wafanyakazi wachache wa China, ambao wanachukua asilimia 10 tu. Tutaendelea kupunguza wafanyakazi wa China, na kuwaajiri wenyeji wa huko, wateja na wasimamizi kimsingi watakuwa wenyeji."

    Ili kuwasaidia wateja wa China na nchi mbalimbali duniani wapate mawe mazuri ya Afrika, na wateja wa Afrika wapate mawe ya rangi mbalimbali ya dunia, kampuni ya WanliStone ikitumia mazingira mazuri ya mji wa Xiamen, imetengeneza mawe kutoka China, Amerika Kusini na Russia, na kupeleka Afrika kupitia bandari ya Xiamen.

    China na Afrika Kusini zote ni nchi za BRICS, zimedumisha uhusiano wa karibu kwenye mambo ya biashara na uwekezaji. Serikali ya mji wa Xiamen imechukua hatua nyingi ili kuwasaidia makampuni ya China ikiwemo WanliStone kuelewa zaidi hali ya uwekezaji katika nchi za BRICS, na kusukuma mbele mawasiliano na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara,. Naibu mkurugenzi wa idara ya biashara ya Xiamen Bibi Zheng Yao anasema,

    "Tumejenga vituo vya mawasiliano vya mji wa Xiamen katika nchi mbili za BRICS, ikiwemo Afrika Kusini na India. Tunatarajia vituo hivi vitasaidia makampuni kuelewa hali ya uwekezaji na biashara ya huko."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako