• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Liverpool yazungumza na Arsenal kuhusu uhamisho wa Alex Oxlade-Chamberlain

  (GMT+08:00) 2017-08-31 08:33:01

  Liverpool wameanza mazungumzo na Arsenal kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati Alex Oxlade-Chamberlain. Mchezaji huyo mwenye miaka 24 alikataa kuhamia Chelsea Jumanne hata baada ya klabu hizo kuafikiana kuhusu uhamisho wake wa pauni milion 40.

  Oxlade-Chamberlain anayechezea timu ya taifa ya England anataka kucheza kama kiungo katika safu ya kati na anahisi kwamba anaweza akapata nafasi Anfield. Alikataa kuhamia Chelsea baada ya kugundua kwamba huenda wakataka kumtumia katika upande wa kushoto uwanjani. Bado haijabainika iwapo Liverpool watafikia dau ambalo Chelsea walikuwa wamewasilisha. Oxlade-Chamberlain anatumikia mkataba wake wa mwisho Emirates na amecheza mechi zote nne za Arsenal msimu huu licha ya kumwambia meneja Arsene Wenger kwamba hatatia saini mkataba mpya. Alishangiliwa na wachezaji wa Liverpool alipoondolewa uwanjani wakati wa mechi ya Jumapili ambayo Arsenal walilazwa 4-0 uwanjani Anfield. Kiungo huyo wa kati ameichezea Arsenal mechi 198 tangu ajiunge nao kutoka Southampton Agosti 2011.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako