• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IOM yarekodi vifo vya wahamiaji 23,000 kote duniani tangu mwaka 2014

    (GMT+08:00) 2017-08-31 08:56:15

    Shirika la uhamiaji la kimataifa IOM limesema vifo vya wahamiaji wapatao 23,000 vimerekodiwa kote duniani tangu mwaka wa 2014. Taarifa iliyotolewa jana na shirika hilo katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu Waliopotea imesema, kwa ujumla vifo vya watu elfu 60 waliopoteza maisha wakiwa kwenye njia ya uhamiaji vimerekodiwa katika miaka 20 iliyopita, na kwamba takwimu hiyo bado sio kamili. Taarifa hiyo inasisitiza kuwa haki za wahamiaji, ikiwemo haki ya kuishi, zinatakiwa kulindwa ili kuhakikisha uhamiaji wao unafanyika salama, kwa utaratibu, kwa heshima na kwa njia ya kibinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako