• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa pande tatu kuhusu kurejesha wakimbizi wa Burundi makwao

    (GMT+08:00) 2017-08-31 09:01:14

    Tanzania, Burundi, na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR zinakutana leo katika mazungumzo yanayolenga kujadili kuwarejesha makwao wakimbizi wa Burundi walioko magharibi mwa Tanzania.

    Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo nchini Tanzania imesema, mazungumzo hayo ya siku moja yatafanyika mjini Dar es Salaam na kuongozwa na waziri wa mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba. Wiki iliyopita, waziri Nchemba aliitaka UNHCR kuanza kuwarejesha wakimbizi zaidi ya elfu nane wa Burundi ambao wamekubali kurudi makwao kwa hiari ndani ya siku saba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako