• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yakana kuwa msuluhishi wa mzozo wa kidiplomasia wa Qatar

    (GMT+08:00) 2017-08-31 09:28:07

    Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw Sergei Lavrov jana amesema kwamba Russia haitakuwa mpatanishi wa mzozo wa kidiplomasia wa Qatar.

    Akizungumza na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani, Bw Lavrov amesema mgogoro huo unatakiwa kutatuliwa chini ya mfumo wa Baraza la ushirikiano wa nchi za ghuba, kwa njia ya kufanya mazungumzo badala ya kutumia kauli za uhasama.

    Kwa upande wake, Bw Mohammed amesema mzozo huo unapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo bila masharti, na bila kuharibu usalama wa Qatar na nchi za ghuba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako