• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Lebanon yatangaza ushindi katika mapambano ya kuliondoa kundi la IS

    (GMT+08:00) 2017-08-31 09:28:46

    Serikali ya Lebanon jana imesema kwamba operesheni ya kijeshi ya kuliondoa kundi la IS kwenye eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, karibu na mpaka wa Syria imemalizika kwa mafanikio.

    Akikutana na wanahabari, Rais Michel Aoun wa Lebanon amesema, nchi hiyo imefanikiwa katika mapambano dhidi ya ugaidi, na kulipongeza jeshi la taifa kwa ushindi wake.

    Kamanda mkuu wa jeshi la Lebanon Brigedia Jenerali Joseph Aoun amesema kazi ya kuliondoa kundi la IS kimemalizika, na kwamba wapiganaji wa kundi hilo wameondolewa nchini humo, na askari tisa waliotekwa nyara na wapiganaji hao wameokolewa.

    Wiki iliyopita, jeshi la Lebanon lilianza operesheni ya kijeshi kaskazini mashariki mwa Lebanon, ambapo makumi ya wapiganaji wa kundi la IS waliangamizwa, na askari saba wa Lebanon pia waliuawa kwenye operesheni hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako