• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wapiganaji 94 wa IS wauawa mkoani Anbar, Iraq

  (GMT+08:00) 2017-08-31 10:01:17

  Wapiganaji 94 wa kundi la IS wameuawa jana kwenye shambulizi lililotokea katika mji unaodhibitiwa na kundi hilo mkoani Anbar, Iraq, karibu na mpaka wa Syria.

  Taarifa iliyotolewa na kamandi ya operesheni ya pamoja ya Iraq imesema, ndege za kivita za nchi hiyo zilishambulia sehemu sita za kundi la IS katika mji wa al-Qaim, kilomita 480 kaskazini magharibi mwa Baghadad, na kuwaua wapiganaji 94 wa IS.

  Ripoti za kijasusi zimethibitisha kuwa, kati ya waliouawa ni pamoja na kiongozi wa usalama wa IS Dhafir al-Rawi, na Mulla Hashim Frahat, mmoja wa watu muhimu wa kundi hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako