• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi halisi ya askari wa Marekani nchini Afghanistan ni kubwa zaidi kuliko iliyotangazwa

    (GMT+08:00) 2017-08-31 16:35:21

    Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema idadi ya askari wa Marekani nchini Afghanistan ni elfu 11, ambayo ni kubwa zaidi kuliko idadi iliyotangazwa na jeshi la Marekani ambayo ni 8400.

    Msemaji wa wizara hiyo Bibi Dana White amesema kutangazwa kwa idadi mpya ni matokeo ya kuongezeka kwa uwazi wa jeshi, na hakumaanishi kwamba Marekani imeongeza askari nchini Afghanistan, na idadi hiyo ni pamoja na askari wanaokaa Afghanistan kwa muda mfupi.

    Tarehe 21 mwezi huu Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza mkakati mpya wa Marekani kuhusu vita nchini Afghanistan, na alisema Marekani itaongeza askari nchini humo, lakini hakudokeza idadi itakayoongezwa. Waziri wa ulinzi wa Marekani amesema idadi hiyo itaamuliwa baada ya kujua idadi halisi ya askari walioko nchini Afghanistan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako