• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano kwenye nishati endelevu

    (GMT+08:00) 2017-08-31 18:19:36

    China na nchi za Afrika zinaendelea kuimarisha ushirikiano kwenye eneo la nishati endelevu, na kuonesha msimamo wa nchi zinazoendelea kutumia fursa kubwa ya nishati safi kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Jumuiya zinazohimiza matumizi ya nishati endelevu na viwanda vya China, wamesaini makubaliano na mpango wa nishati endelevu wa Afrika AREI, yatakayowezesha makampuni ya nishati endelevu ya China na viwanda, kutoa teknolojia na uungaji mkono wa kifedha kwa nchi za Afrika.

    Baadhi ya miradi itakayohusishwa kwenye makubaliano hayo ni pamoja na gridi ndogo za umeme kwenye kaya na vijiji, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vikubwa vya kusambaza umeme.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako