• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya watu 500 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameomba hifadhi nchini Zambia

    (GMT+08:00) 2017-08-31 18:19:56

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema zaidi ya watu 500 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wameomba hifadhi nchini Zambia katika siku moja, na kufanya idadi hiyo iwe idadi kubwa zaidi kwa wakimbizi kuomba hifadhi ndani ya siku moja.

    Mwakilishi wa UNHCR nchini Zambia Bibi Pierrine Aylara amesema watu hao wamehifadhiwa na jamii za wenyeji, na hadi sasa wamekuwa wakiendelea kupokea mawimbi ya wakimbizi kutoka DRC. Kwa sasa UNHCR inaendelea kushirikiana na jamii za wenyeji kuhesabu wakimbizi wanaoingia

    Takwimu za UNHCR zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 3000 kutoka DRC wameomba hifadhi nchini Zambia kuanza mwezi Januari hadi mwezi Agosti, na katika mwezi Agosti peke yake watu waliomba hifadhi ni watu 1000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako