• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan kusini: Serikali ya Sudan Kusini yatafuta mikopo kufadhili bajeti

    (GMT+08:00) 2017-08-31 19:17:30

    Serikali ya Sudan Kusini imepitisha bajeti ya dola milioni 300 ya mwaka wa 2017/2018 lakini imesema itategemea mikopo kufadhili sehemu kubwa ya bajeti hiyo.

    Wabunge walipiga kura kunga mkono pendekezo la kuwa na ongezeko la zaidi ya asilimia 30 ya pesa za matumizi na hivyo kupandisha bajeti hiyo.

    Katibu kwenye wizara ya fedha Wani Buyu Dyori, amewaambia waandishi wa habari mjini Juba kwamba serikali itakuwa na ugumu wa kufadhili bajeti hiyo.

    Sekta zinazoshukua kiasi kikubwa cha fedha ni kama vile usalama ambayo itapata asilimia 27 ya bajeti yote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako