• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Watalii kufurika Rwanda wakati wa "Kwita Izina"

    (GMT+08:00) 2017-08-31 19:18:12

    Rwanda inatarajiwa kupokea watalii wengi wa kigeni na wale wa ndani wakati wa hafla ya kila mwaka ya kuwapa Sokwe majina maarufu kama Kwita Izina.

    Mkurungezi wa halmashauri ya maendeleo nchini humo Clare Akamazi amesema kesho hafla hiyo itaanza kwenye eneo la Kinigi wilaya ya Musanze katika hifadhi ya kitaifa kwenye milima ya Volkano.

    Mwaka huu sokwe 19 watapewa majina hii ikiwa ni juhudi za kuwahifadhi wanayam hao.

    Kuna sokwe 800 tu wa milimani waliosalia kote duniani na Rwanda kuna 400 kati ya hao.

    Tangu hafla hiyo ianze miaka 13 iliopita sasa sokwe 239 wamepewa majina.

    Sokwe wa milimani huchangia asilimia 90 ya mapato ya serikali kutoka kwa hifadhi za kitaifa,

    Mwaka 2016 Rwanda ilipata dola milioni 404 kutoka kwa utalii na mwaka huu inalenga dola milioni 444.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako