• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: IPTL yanyimwa leseni na EWURA

    (GMT+08:00) 2017-08-31 19:18:26

    Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini Tanzania (EWURA, imekataa kuiongezea muda wa leseni Kampuni ya Kufua Umeme wa Independent Power Tanzania Limited (IPTL) baada ya leseni yake ya kuzalisha umeme kumalizika muda wake.

    Kwa mujibu wa tangazo la Ewura, lililotolewa kama taarifa kwa vyombo vya habari na kuchapishwa ndani ya gazeti hili, maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Ewura kilichofanyika Agosti 30, mwaka huu.

    Taarifa hiyo ilieleza kuwa Machi 28, mwaka huu, Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) iliwasilisha kwa Ewura maombi ya kuongeza muda wa leseni ya kuzalisha umeme kwa miezi 55 kuanzia Julai 16, 2017 hadi Januari 15, 2022.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako