• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia: Shirika la ndege la Ethiopia lajadili na Nigeria kununua shirika la Arik Air.

    (GMT+08:00) 2017-08-31 19:18:43

    Shirika la ndege la Ethiopia linajadili na serikali ya Nigeria kununua shirika la ndege lililofilisika la Arik Air.

    Mkurungezi wa huduma za kimataifa kwenye shirika hilo la Ethiopia Esayas Weldemariam, amesema wanapanua oparesheni zao magharibi mwa Afrika.

    Amesema kwa kufuata ofa ya serikali ya Nigeria wametuma maombi yao miongoni mwa mashirika mengine.

    Arik Air, ni mojawepo wa mashirika makubwa zaidi ya kibinafsi nchini Nigeria na limekuwa likuhudumu kama shirika la ndege la kitaifa.

    Shirika la ndege la Ethiopia ni mojawepo wa yale yenye ufanisi zaidi barani Afrika likiwa na ndege 92 na kuhudumu katika miji 104 kimataifa na miji 14 ndani ya Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako