• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Kenya wawakamata wahamiaji haramu 13 kutoka Ethiopia

    (GMT+08:00) 2017-08-31 19:25:55

    Polisi wa Kenya wanawahoji wahamiaji haramu 13 kutoka Ethiopia baada ya kuwakamata kwenye jengo mmoja mjini Nairobi.

    Kamanda wa polisi wa kaunti ya Nairobi Bw Joseph Koome amesema watu hao walikamatwa jana usiku, na kusema msako dhidi ya mtu aliyekuwa anawasafirisha unaendelea, na watu hao waliokamatwa watarudishwa kwao.

    Polisi walipewa taarifa na watu kuhusu kundi la watu wasiojua kiingereza wala Kiswahili, ambao wanaaminika walikuwa wanakuja kwenye makundi madogo madogo.

    Polisi wa Kenya wamekuwa wakiwakamata wahamiaji haramu kutoka Ethiopia, ambao wanapita kuelekea Tanzania na Afrika Kusini. Wengi wanakamatwa kwenye vyumba vidogo vilivyosongamana kwenye miji mbalimbali ya Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako