• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa BRICS watarajiwa kupata matokeo katika kuimarisha ushirikiano kifedha

    (GMT+08:00) 2017-08-31 20:50:07

    Mkutano wa nchi za BRICS utakaofanyika hivi karibuni mjini Xiamen, China unatarajiwa kupata matokeo mazuri katika kuhimiza ushirikiano wa mambo ya kifedha, yatakayotoa mchango mpya kwa ajili ya kuendeleza uchumi wa nchi za BRICS na dunia nzima. Pia kukamilisha utawala wa uchumi wa dunia, na kuinua zaidi kiwango cha ushirikiano halisi kati ya nchi za BRICS.

    Akizungumza na waandishi wa habari hii leo, mkurugenzi wa kituo cha mambo ya kifedha ya kimataifa kilicho chini ya wizara ya fedha ya China Bw. Zhou Qiangwu amesema, katika miaka 10 iliyopita, nchi tano wanachama wa BRICS zimepanua na kukamilisha ushirikiano kwa kufuata kanuni ya kufungua mlango, kusikilizana, kushirikiana na kupatia mafanikio ya pamoja. Hivi sasa mfumo wa BRICS ni jukwaa muhimu la kuendeleza mazungumzo na ushirikiano kati ya nchi kubwa zinazoendelea na utawala wa uchumi wa dunia, pia ushawishi na mvuto wake unaongezeka siku hadi siku.

    "Licha ya mkutano wa viongozi, nchi za BRICS zinafanya mazungumzo zaidi ya 20 kila mwaka. Hapa China wizara na idara kuu zaidi ya 40 za serikali zimeshiriki mfumo wa ushirikiano wa BRICS. Ushirikiano wa mambo ya kifedha ni sehemu muhimu ya mfumo wa BRICS. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi za BRICS zimeongeza mawasiliano na uratibu katika suala la kifedha, na kupata matokezo mazuri. Hali ambayo imetoa mchango muhimu kwa ajili ya kuendeleza uchumi na jamii ya nchi za BRICS na kukamilisha utawala wa dunia."

    Bw. Zhou Qiangwu ameeleza kuwa, mkutano huo utafikia makubaliano mengi kuhusu ushirikiano wa mambo ya kifedha. Anasema,

    "Ili kuhimiza maendeleo ya uchumi wa nchi za BRICS na dunia nzima, nchi tano wanachama wa BRICS zitaongeza mawasiliano na uratibu kati ya serikali, na kutumia zana zote za sera. Nchi hizo zitazihimiza nchi zilizoendelea kutekeleza sera inayojiwajibisha ya uchumi, na kupunguza athari mpya kwa nchi nyingine. Aidha tutafafanua msimamo wetu wa kupinga vitendo vya kujilinda kibiashara." Hivi sasa mchakato wa kufufuka kwa uchumi wa dunia unakabiliwa na changamoto nyingi, zikiwemo vitendo vinavyokiuka utandawazi wa dunia na juhudi za kulinda mazingira. Ili kukabiliana na changamoto hizo, mkurugenzi wa idara ya utafiti wa uchumi wa dunia iliyo chini ya kamati kuu ya mageuzi ya maendeleo ya China Bw. Ye Fujing amependekeza nchi za BRICS kuimarisha ushirikiano zaidi. Anasema,

    "Nchi hizi zinapaswa kutunga na kutekeleza mpango wa ushirikiano wa kibiashara, uchumi na uwekezaji kabla ya mwaka 2020, na kufikiria kutekeleza sera ya biashara na uwekezaji ya kunufaishana, na kupunguza ushuru wa forodha bila ya kukiuka ahadi za Shirika la Biashara Duniani, ili kupata matokeo halisi ya awali kabla ya kujenga eneo la biashara huria kati ya nchi za BRICS."

    Wataalamu wanaeleza kuwa mkutano wa viongozi wa nchi za BRICS wenye kauli mbiu ya kukuza uhusiano wa kiwenzi kati ya nchi za BRICS, na kuanzisha mustakabali mzuri zaidi, unalengea kuhimiza maendeleo ya nchi za BRICS, kutimiza ushirikiano na mafanikio ya pamoja kati ya nchi zinazoendelea. Pia kujenga utaratibu wazi wa uchumi wa dunia, kukalimisha utawala wa dunia, na kutatua matatizo ya ukosefu wa amani, maendeleo na utawala kwa njia ya kuongeza ushirikiano wa kiwenzi kati ya nchi za BRICS. Aidha, nchi za BRICS pia zitahimiza kuendeleza na kukamilisha akiba ya kukabiliana hali ya dharura, soko la dhamana, na mitandao ya mashirika na huduma za kifedha. Nchi hizo pia zitaongeza mawasiliano na ushirikiano katika usimamizi wa mambo ya kifedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako