• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chirwa, Kaseke na Msuva wapewa onyo kali na TFF

  (GMT+08:00) 2017-09-01 08:43:27

  Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemruhusu kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa kuendelea kucheza Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara baada ya kumpa onyo kali kwa kosa la kumghasi refa. Hayo yamefikiwa katika kikao cha kamati hiyo na uamuzi huo unamnufaisha pia kiungo mpya wa Singida United, Deus Kaseke.

  Hata hivyo kamati hiyo imetangaza kumuandikia barua ya onyo kali winga mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na club ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva kwa kosa la kumsukuma muamuzi wakati akiwa Yanga.

  Msuva ambaye alikuwa anatuhumiwa kufanya kosa hilo akiwa pamoja na wenzake Deus Kaseke na Obrey Chirwa, yeye pekee ndio amekutwa na hatia wakati Kaseke na Chirwa hawajakutwa na hatia ya kutenda kosa hilo.

  Lakini refa, Ludovic Charles naye alipewa onyo kali kwa kutoumudu mchezo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako