• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashirikiana na WFP kupambana na njaa nchini Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2017-09-01 08:47:53

    Serikali ya China inaimarisha ushirikiano na Shirika la mpango wa chakula la umoja wa mataifa WFP kuziwezesha jamii za vijijini nchini Zimbabwe kujitegemea kwa chakula na kuhimili madhara yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Tangu mwaka 2009, serikali ya China kupitia WFP imekuwa ikiipatia serikali ya Zimbabwe msaada wa fedha kwa ajili ya msaada wa dharura wa chakula, na msaada wa muda mrefu ili kujenga uwezo kwa jamii zilizohatarini, kwenye maeneo maskini Zimbabwe.

    Katika muda wa miaka kumi iliyopita China imeipatia Zimbabwe msaada wa dharura wa mamilioni ya dola, mashine za kilimo pamoja na mbolea.

    Wiki hii serikali ya China imetangaza kuipatia Zimbabwe dola milioni 5 za kimarekani kupitia WFP kuwasaidia wakimbizi na kujenga uwezo kwa jamii zilizo hatarini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako