• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazindua pasipoti ya kielektroniki kurahisha watu kuvuka mpaka na biashara

    (GMT+08:00) 2017-09-01 08:48:40

    Kenya imezindua pasipoti ya kielektroniki ili kuongeza ufanisi, usalama na ufuatiliaji wa watu wanaovuka mpaka na bidhaa.

    Kaimu waziri wa mambo ya ndani Bw Fred Matiang'i amesema kuzinduliwa kwa pasipoti hiyo kuendana na ahadi ya Kenya ya kuhimiza mafungamano ya kikanda kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.

    Kenya imekuwa ni nchi ya pili baada ya Burundi kutoa pasipoti ya aina hiyo, uamuzi ambao ulifikiwa na nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki mwezi machi mwaka 2016.

    Bw Matiang'i amesema pasipoti hiyo ni salama sana na vigumu kugushi, na imetolewa wakati Kenya inapambana na ugaidi na biashara ya magendo ya binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako