• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO yasaidia wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Uganda kuongeza uzalishaji wa chakula

    (GMT+08:00) 2017-09-01 09:06:34

    Mkuu wa shirika la chakula Duniani FAO Bw Jose Graziano da Silva amesema shirika hilo litaendelea kuwaunga mkono wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Uganda kuongeza uzalishaji wa chakula.

    Bw. Silva amesema ni vigumu kuongeza uzalishaji wa chakula kwa wakimbizi baada ya kupungua kwa msaada wa kibinadamu. Amesema shirika lake litatoa mbegu ya mimea inayokomaa haraka kwa wakimbizi hao na kuwapa uwezo wa kilimo.

    Bw. Silva amemaliza ziara yake kwenye kambi ya wakimbizi wa Sudan Kusini iliyoko kaskazini mwa Uganda, ambapo alizindua mradi wa umwagiliaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako