• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yaitaka Marekani kuondoa vikwazo dhidi yake kwa wakati uliopangwa

    (GMT+08:00) 2017-09-01 09:07:14

    Sudan imesema inatarajia kuwa Marekani itaondoa kikamilifu vikwazo vya kiuchumi dhidi yake baada ya muda wa nyongeza wa tathimini kumalizika Oktoba.

    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw Ibrahim Ghandour aliyasema hayo alipokutana na ujumbe wa Marekani huko Khartoum.

    Amesema Sudan inajitahidi kutekeleza mambo waliyoafikiana na itaendelea na ushirikiano katika suala hilo, na kusubiri Marekani itekeleze ahadi yake na kuondoa vikwazo dhidi ya Sudan mwezi Oktoba.

    Ujumbe wa Marekani pia umeeleza nia ya serikali ya Marekani ya kushirikiana na Sudan kuhusu suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako